Matthew 5

Mahubiri Ya Isa Kwenye Mlima

(Mathayo 5–7)

Sifa Za Aliyebarikiwa

(Luka 6:20-23)

1 aBasi Isa alipoona makutano, alipanda mlimani akaketi chini, nao wanafunzi wake wakamjia. 2Ndipo akaanza kuwafundisha, akisema:
3 b“Heri walio maskini wa roho,
maana Ufalme wa Mbinguni ni wao.

4 cHeri wale wanaohuzunika,
maana hao watafarijiwa.

5 dHeri walio wapole,
maana hao watairithi nchi.

6 eHeri wenye njaa na kiu ya haki,
maana hao watatoshelezwa.

7 fHeri wenye huruma,
maana hao watapata rehema.

8 gHeri walio na moyo safi,
maana hao watamwona Mungu.

9 hHeri walio wapatanishi,
maana hao wataitwa wana wa Mungu.

10 iHeri wanaoteswa kwa sababu ya haki,
maana Ufalme wa Mbinguni ni wao.

11 j“Heri ninyi watu watakapowashutumu, na kuwatesa na kunena dhidi yenu mabaya ya aina zote kwa uongo kwa ajili yangu. 12 kFurahini na kushangilia kwa maana thawabu yenu ni kubwa mbinguni, kwa kuwa hivyo ndivyo walivyowatesa manabii waliokuwa kabla yenu.

Chumvi Na Nuru

(Marko 9:50; Luka 14:34-35)

13 l“Ninyi ni chumvi ya ulimwengu. Lakini chumvi ikipoteza ladha yake, yawezaje kurudishiwa ladha yake tena? Haifai tena kwa kitu chochote, ila kutupwa nje ikanyagwe na watu.

14 m“Ninyi ni nuru ya ulimwengu. Mji uliojengwa kilimani hauwezi kufichika. 15 nWala watu hawawashi taa na kuifunika kwa bakuli. Badala yake, huiweka kwenye kinara chake, nayo hutoa mwanga kwa kila mtu aliyemo ndani ya ile nyumba. 16 oVivyo hivyo, nuru yenu iangaze mbele ya watu, ili wapate kuona matendo yenu mema wamtukuze Baba yenu aliye mbinguni.

Kutimiza Sheria

17 p“Msidhani kwamba nimekuja kufuta Torati au Manabii; sikuja kuondoa bali kutimiza. 18 qKwa maana, amin nawaambia, mpaka mbingu na dunia zitakapopita, hakuna hata herufi moja ndogo wala nukta itakayopotea kwa namna yoyote kutoka kwenye Torati, mpaka kila kitu kiwe kimetimia. 19 rKwa hiyo, yeyote atakayevunja mojawapo ya amri ndogo kuliko zote ya amri hizi, naye akawafundisha wengine kufanya hivyo, ataitwa mdogo kabisa katika Ufalme wa Mbinguni, lakini yeyote azitendaye na kuzifundisha hizi amri ataitwa mkuu katika Ufalme wa Mbinguni. 20 sKwa maana nawaambia, haki yenu isipozidi haki ya Mafarisayo na walimu wa sheria, kamwe hamtaingia katika Ufalme wa Mbinguni.

Kuhusu Hasira

(Luka 12:57-59)

21 t“Mmesikia walivyoambiwa watu wa zamani kwamba, ‘Usiue. Yeyote atakayeua atapaswa hukumu.’ 22 uLakini mimi nawaambia kwamba, yeyote atakayemkasirikia ndugu yake, atapaswa hukumu. Tena, yeyote atakayemwambia ndugu yake, ‘Raka,’
Raka ni neno la Kiaramu ambalo maana yake ni dharau au dhihaka ya hali ya juu.
atapaswa kujibu kwa Baraza la Wayahudi.
Baraza la Wayahudi lilikuwa kundi kuu kabisa la utawala wa Wayahudi lililoundwa na wazee 70 pamoja na kuhani mkuu.
Lakini yeyote atakayesema ‘Wewe mpumbavu!’ atapaswa hukumu ya moto wa jehanamu.

23 x“Kwa hiyo, kama unatoa sadaka yako madhabahuni, ukakumbuka kuwa ndugu yako ana kitu dhidi yako, 24 yiache sadaka yako hapo mbele ya madhabahu. Enda kwanza ukapatane na ndugu yako; kisha urudi na ukatoe sadaka yako.

25 z“Patana na mshtaki wako upesi wakati uwapo njiani pamoja naye kwenda mahakamani, ili mshtaki wako asije akakutia mikononi mwa hakimu, naye hakimu akakutia mikononi mwa askari, nawe ukatupwa gerezani. 26Amin, nakuambia, hautatoka humo hadi uwe umelipa senti ya mwisho.

Kuhusu Uzinzi

27 aa“Mmesikia kwamba ilinenwa, ‘Usizini.’ 28 abLakini mimi nawaambia kwamba, yeyote amtazamaye mwanamke kwa kumtamani, amekwisha kuzini naye moyoni mwake. 29 acJicho lako la kuume likikusababisha kutenda dhambi, ling’oe ulitupe mbali. Ni afadhali kwako kupoteza kiungo kimoja cha mwili wako kuliko mwili wako mzima ukatupwa jehanamu. 30 adKama mkono wako wa kuume ukikusababisha kutenda dhambi, ukate, uutupe mbali. Ni afadhali kwako kupoteza kiungo kimoja cha mwili wako kuliko mwili wako mzima utupwe jehanamu.

Kuhusu Talaka

(Mathayo 19:9; Marko 10:11-12; Luka 16:18)

31 ae“Pia ilinenwa kwamba, ‘Mtu yeyote amwachaye mkewe sharti ampe hati ya talaka.’ 32 afLakini mimi nawaambia, yeyote amwachaye mkewe isipokuwa kwa kosa la uasherati, amfanya mkewe kuwa mzinzi. Na yeyote amwoaye yule mwanamke aliyeachwa, anazini.

Kuhusu Kuapa

33 ag“Tena mmesikia walivyoambiwa watu wa zamani kwamba, ‘Usiape kwa uongo, bali timiza kiapo kile ulichofanya kwa Bwana.’ 34 ahLakini mimi nawaambia, msiape kabisa: iwe kwa mbingu, kwa kuwa ni kiti cha enzi cha Mungu; 35 aiau kwa dunia, kwa kuwa ndipo mahali pake pa kuwekea miguu; au kwa Yerusalemu, kwa kuwa ndio mji wa Mfalme Mkuu. 36Nanyi msiape kwa vichwa vyenu, kwa kuwa hamwezi kuufanya hata unywele mmoja kuwa mweupe au mweusi. 37 aj‘Ndiyo’ yenu iwe ‘Ndiyo,’ na ‘Hapana’ yenu iwe ‘Hapana.’ Lolote zaidi ya hili latoka kwa yule mwovu.

Kuhusu Kulipiza Kisasi

(Luka 6:29-30)

38 ak“Mmesikia kwamba ilinenwa, ‘Jicho kwa jicho na jino kwa jino.’ 39 alLakini mimi nawaambia, msishindane na mtu mwovu. Lakini kama mtu akikupiga kwenye shavu la kuume, mgeuzie na la pili pia. 40 amKama mtu akitaka kukushtaki na kuchukua joho lako, mwachie achukue na koti pia. 41 anKama mtu akikulazimisha kwenda maili moja, nenda naye maili mbili. 42 aoMpe yeye akuombaye, wala usimgeuzie kisogo yeye atakaye kukukopa.

Upendo Kwa Adui

(Luka 6:27-28, 32-36)

43 ap“Mmesikia kwamba ilinenwa, ‘Mpende jirani yako na umchukie adui yako.’ 44 aqLakini ninawaambia: Wapendeni adui zenu na waombeeni wanaowatesa ninyi, 45 arili mpate kuwa watoto wa Baba yenu aliye mbinguni. Kwa maana yeye huwaangazia jua lake watu waovu na watu wema, naye huwanyeshea mvua wenye haki na wasio haki. 46 asKama mkiwapenda tu wale wanaowapenda, mtapata thawabu gani? Je, hata watoza ushuru hawafanyi hivyo? 47Nanyi kama mkiwasalimu ndugu zenu tu, je, mnafanya nini zaidi ya wengine? Je, hata watu wasiomjua Mungu, hawafanyi hivyo? 48 atKwa hiyo kuweni wakamilifu kama Baba yenu wa mbinguni alivyo mkamilifu.
Copyright information for SwhKC